Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele aitikisa kambi ya Monastir

Mayele Fr ..jpeg Mayele

Wed, 15 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa kati wa US Monastir, Ousmane Outtara amesema kuwa wao binafsi wana hofu na wapinzani wao Yanga haswa katika uwanja wao wa nyumbani, Benjamin Mkapa ambapo wamepata ushindi katika michezo yao yote.

Outtara ambaye amewahi kucheza katika klabu ya AS Vita ya DR Congo pia ameeleza ugumu wa kumkaba Mayele katika mchezo wa kwanza ambao walikutana.

Hadi sasa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga wamecheza mechi mbili kwenye uwanja huo wa Mkapa dhidi ya TP Mazembe na Real Bamako ambapo mechi zote hizo wamefanikiwa kushinda. Waliwafunga Mazembe 3-1 na Bamako 2-0.

Jumapili hii Yanga kwa mara nyingine watakuwa kwenye uwanja huo kucheza na US Monastir ya Tunisia ambapo Yanga wanahitaji pointi tatu kusonga hatua ya robo fainali kutoka kwenye msimamo wa kundi D ambapo hadi sasa wapo nafasi ya pili na pointi saba.

Mayele aitikisa kambi ya Monastir Akizungumza na Championi Jumatatu, Outtara alisema: “Ninaufahamu vyema Uwanja wa Mkapa, nimewahi kwenda pale na AS Vita, kule watu wanapenda sana mpira na ni ngumu kupata matokeo kirahisi.

“Yanga wamepata ushindi katika michezo miwili mfululizo hivyo naamini tunakwenda kukutana na changamoto pale, siyo rahisi kupata matokeo lakini naamini tumejiandaa vyema kupata matokeo mazuri.

“Mayele ni mchezaji mzuri sana, ni mshambuliaji ambaye amekamilika, anafunga kila aina ya bao ambalo mshambuliaji anatakiwa kufunga.

“Katika mchezo uliopita tulifanikiwa kucheza naye lakini haikuwa rahisi, najua tukiwa ugenini pia tutakutana na mtihani wa kukabiliana naye, lakini tutapambana naye ili asitusumbue,” alisema beki huyo.

Akizungumza nasi, Mayele alisema, kila mchezo ni muhimu kwao lakini kwa upande wa kimataifa ni muhimu zaidi kwa sasa kwa sababu imebaki mechi mbili ambazo zinatakiwa kutuweka sisi kwenye levo nyingine.

“Ukitazama kwenye ligi kuna mechi nyingi kidogo ambazo tukipambana zaidi tutakuwa mabingwa. Ila huku kwenye shirikisho tuna mechi mbili ambazo zitaamua hatma yetu.

“Naiwaza zaidi timu yangu kwa sasa ili iweze kufanikiwa kwenye kila hatua na kisha nawaza mimi pia malengo yao niliyojiwekea, kwenda robo fainali shirikisho ni mipango ya timu na mimi pia,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: