Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele aionya Simba SC

Mayele Baleke Mayele aionya Simba SC

Wed, 12 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuiongoza Yanga kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold na kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC), straika Mkongomani wa Yanga, Fiston Mayele amechimba mkwara mzito kuwa hakuna wa kuwazuia kushinda ubingwa wa mashindano hayo.

Mayele akitokea benchi na kucheza kwa dakika 45 tu, kwenye mchezo huo uliopigwa siku ya Jumamosi aliifungia Yanga bao pekee la ushindi na sasa Yanga wanatarajiwa kuvaana na Singida Big Stars katika mchezo wa nusu fainali utakaopigwa kwenye Uwanja wa Liti mkoani Singida.

Akizungumza nasi, Mayele alisema: “Ni jambo zuri kwetu kuona timu imefanikiwa kufuzu nusu fainali ya mashindano haya, tulishinda ubingwa msimu uliopita na malengo yetu makubwa ni kuhakikisha tunashinda tena msimu huu.

“Tunafahamu Singida ni timu ngumu tulicheza nao kwenye Ligi Kuu Bara na licha ya kwamba tulishinda lakini ulikuwa mchezo mgumu na wao wamethibitisha ubora wao kwa kuangalia msimamo wa Ligi Kuu mpaka sasa, lakini tunaamini hakuna anayeweza kutuzuia kushinda ubingwa kutokana na ubora wa kikosi chetu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: