Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele afichua jambo Yanga

Mayele 763318 Fiston Kalala Mayele

Sat, 1 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Kalala Mayele, amesema kuwa kwa sasa Yanga inaogopwa na mashabiki wengi waliopo nchini DR Congo kutokana na ushindi wa kwanza walioupata nyumbani Uwanja wa Mkapa, Dar.

Mayele kwa sasa yupo nchini huko akiwasubiri Yanga ambao wataenda kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya TP Mazembe utakaofanyika kesho Aprili 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa TP Mazembe uliopo Lubumbashi, DR Congo.

Akizungumza nasi, Mayele alisema, kwa sasa nchini DR Congo, Yanga inaheshimika, lakini pia inaogopwa na mashabiki wengi kutokana na ushindi ambao iliupata katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Mkapa, pia kutokana na ubora ambao Yanga imekuwa inauonesha.

“Kwa sasa Yanga inaheshimika sana huku DR Congo, hiyo ni kutokana na ubora mkubwa ambao timu imezidi kuuonesha na ukubwa wa timu kuzidi kuongezeka kila wakati.

“Ushindi ambao tuliupata dhidi ya TP Mazembe tukiwa Dar umezidi kuwafanya mashabiki wa huku kuihofia zaidi Yanga, huku pia watu wakienda mbali zaidi kwa kuipa nafasi kubwa Yanga kupata matokeo mazuri katika mchezo wetu wa pili wa marudiano tukiwa hapa.

“Kikubwa sisi kama wachezaji tayari tumejiwekea malengo yetu ambayo yalikuwa ni kuhakikisha tunapata matokeo mazuri katika mchezo huo ili tujihakikishie nafasi ya kuongoza kundi, lakini kuwaonesha ndugu zetu waliopo huku kuwa tunafanya kazi nzuri ndani ya Yanga,” alisema mshambuliaji huyo.

Ikumbukwe kuwa, katika mchezo uliochezwa Februari 19, mwaka huu Uwanja wa Mkapa, Dar, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: