Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele: Yanga ndio wataamua hatma yangu

Mayele37520 Fiston Mayele

Tue, 20 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga SC, Fiston Mayele amesema kuwa hatima yake ndani ya klabu hiyo itaamriwa na Yanga wenyewe.

Kauli hiyo ya Mayele ameitoa kupitia InstaStory yake kufuatia tetesi kuwa anatakiwa na vilabu mbalimbali barani Afrika na nje ya Afrika ambao wamemtengea kitita kirefu kumng'oa Jangwani.

Kwa sasa Mayele yupo kwenye majukumu na Timu yake ya Taifa ya Congo DR ambapo juzi aliifungia bao la pili dhidi ya Gabon katika ushindi wa 2-0.

"Watu wanasubiria THANK YOU ya kwangu ila hatima yangu ipo chini ya viongozi wa Yanga SC.

"Hivi sasa niko katika majukumu ya timu ya taifa, lakini nitarudi Tanzania maana familia yangu iko huko, najua watu wengi wanasubira neno hilo ambalo kwa sasa limekuwa maarufu Tanzania," amesema Mayele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: