Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele: Yanga kwanza, mimi baadaye

Mayele Hdfsgs.jpeg Mayele Fiston

Tue, 30 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Straika wa Yanga, Fiston Kalala Mayele ameeleza lengo lake kubwa msimu huu ni kuhakikisha kwanza Yanga inabeba makombe kisha ndio awaze kuhusu yeye kuwa mfungaji bora.

Mpaka sasa Mayele ni kinara wa mabao kwenye Ligi ya NBC akiwa amefunga mabao 16 huku akiongoza pia kwenye Kombe la Shirikisho akipachika mabao 7 mpaka sasa.

“Ndoto yangu msimu huu ni kubeba makombe mengi nikiwa na Yanga, tayari tumeshanyakua ubingwa wa Ligi na sasa nguvu tumezihamishia kwenye Fainali ya CAF na ASFC.

“Nataka niisaidie timu yangu kubeba ubingwa kisha ndio nianze kungalia kuhusu tuzo binafsi, nitahakikisha nafunga mabao ya kutosha ya kuibeba timu yangu,” alisema Mayele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: