Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele: Tunalitaka kombe tena

Fiston Kalala Mayele Tt Fiston Mayele

Wed, 12 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele amesema kuwa kazi kubwa ambayo wataifanya ni kushirikiana kusaka ushindi mpaka kutwaa taji la Azam Sports Federation.

Yanga ni mabingwa watetezi wakiwa wametinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa bao 1-0 Geita Gold uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Mayele alifunga bao pekee la ushindi dhidi ya Geita Gold ambalo limeipa nafasi ya kutinga nusu fainali na inatarajiwa kumenyana na Singida Big Stars katika hatua ya nusu fainali.

Mayele amesema: “Tuna kazi kubwa ya kufanya katika Azam Sports Federation na kufika hatua ya nusu fainali haikuwa kazi nyepesi tunahitaji kupambana ili kutwaa taji hilo.

“Ushindi wetu dhidi ya Geita Gold unatupa nafasi kutinga hatua ya nusu fainali na tutapambana na Singida Big Stars ambayo ni timu imara kwani kwenye ligi inafanya vizuri.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: