Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele: Tuna kazi ngumu, lakini tutatoboa

MAYELE TRE.jpeg Mayele: Tuna kazi ngumu, lakini tutatoboa

Tue, 16 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa kinara wa Klabu ya Yanga, Fiston Mayele amesema kuwa anafahamu ubora wa wapinzani wao Marumo Gallants, hivyo wamejiandaa kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo wao wa kesho.

Mayele amesema hayo kuelekea mchezo wao dhidi ya Marumo kuwania kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika ambapo Yanga ilishinda mchezo wa kwanza kwa bao 2-0 katika Dimba la Mkapa.

Young Africans inatarajia kushuka kwenye Uwanja wa Royal Bafokeng kesho Jumatano (Mei 17) kupambana na Marumo Gallants, huku mchezo huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa.

Mayele, ambaye hadi sasa amepachika mabao matano akishika nafasi ya kwanza katika orodha ya wafungaji sambamba na Ranga Chivaviro, kila mmoja amepachika mabao matano.

Amesema hivi sasa akili yake ipo katika mchezo wa Marumo Gallants, ambao ni muhimu kwao ili kujiweka katika hatua nzuri ya kutinga hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

"Tunatambua tuna kazi ngumu kwani wapinzani wetu ni wazuri na pia wapo kwao. Tumeshatwaa ubingwa wa ligi ni zamu ya kutafuta ubingwa wa Afrika.

"Muhimu ni kupambana tuweze kufika fainali na tukivuka hapo naamini hata kombe tutabeba kwani nakiamini kikosi chetu," amesema Mayele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: