Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele: Nataka pesa tu!

Mayele Mhd.jpeg Fiston Mayele

Fri, 23 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Yanga Mkongomani, Fiston Mayele alipishana na kocha wake Mtunisia, Nasreddine Nabi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wa Jijini Dar es Salaam.

Nabi alikuwa anaondoka nchini kureja kwao Tunisia baada ya kumaliza mkataba wake Yanga huku Mayele naye akitajwa kuwa huenda akaondoka katika timu hiyo kwenye dirisha hili kubwa la usajili.

Mayele na Nabi wanahusishwa kuhitajika na klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ambayo ipo tayari kutoa kitita kikubwa cha fedha kufanikisha mipango hiyo.

Tukio hilo la aina yake lilitokea kwenye uwanja huo wa ndege, wakati mshambuliaji huyo anatua nchini akitokea Gabon ambako alikuwa na kikosi cha timu ya Taifa ya DR Congo ambako alikwenda katika majukumu ya mechi za kimataifa.

Mayele katika timu ya taifa ya DR Congo amefanikiwa kufunga bao moja katika michezo miwili ambayo amecheza, akiwatungua Gabon kwa shuti kali dakika ya 83.

Mara baada ya kutua hapo, Mayele akiwa na familia yake ikiongozwa na mke na watoto wake watatu alikutana na Nabi ambaye alikuwa akirejea nyumbani kwao Tunisia mara baada ya kumalizana na Yanga.

Wakiwa kwenye uwanja huo wa ndege, Nabi alipata nafasi ya kuagana na Mayele ambao walipiga picha za pamoja.

Mayele amerejea nchini kwa ajili ya kufanya mazungumzo na uongozi wa Yanga, katika kufikia muafaka mzuri wa kubakia au kuondoka hapo.

Baada ya kuagana Mayele, aliposti picha akiwa na familia yake akiandika ujumbe mfupi uliosomeka kuwa “Safari njema profesa”.

MAYELE ANATAKA PESA

Kabla ya kutua Bongo, Mayele alizungumza na Championi Jumatano na kuweka wazi kuwa anachokiangalia kwa sasa ni pesa na wala sio jambo jingine.

Akizungumza juu ya hatma yake ya kubakia ndani ya Yanga, Mayele alisema kuwa: “Wananchi msiwe na wasiwasi baada ya kumaliza majukumu yangu ya timu ya taifa nimerudi rasmi Tanzania kwa ajili ya kuhakikisha kuwa naendelea na majukumu yangu, niwaambie tu kwamba mimi ni mwananchi.

“Suala la kubakia Yanga kwangu niwaambie tu wananchi wote limebaki kwa uongozi wa Yanga wao ndio wanafahamu kama nitabaki au nitaondoka Yanga hivyo kwangu mimi nachokiangalia zaidi ni pesa tu wala sio jambo lingine,” alisema Mayele.

Straika huyo anatarajiwa kucheza michezo miwili ya hisani kupitia tamasha la Feisal Salum aliloandaa huko visiwani Zanzibar kisha katika mchezo kati ya Kibwana Shomari na Dickson Job mechi itakayopigwa katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: