Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele: Huu ni msimu bora kwangu tangu nianze soka

MAYELE TRE.jpeg Mayele: Huu ni msimu bora kwangu tangu nianze soka

Mon, 22 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji kinara wa Yanga, Fiston Mayele amesema kuwa msimu huu umekuwa bora sana kwake tofauti ni msiimu yote aliyowahi kucheza soka tangu azaliwe.

Mayele ambaye ni raia wa Congo DR amesema hayo mara baada ya kuifunga Singida Big Stars na kuisaidia Yanga kutinga fainali ya Kombe la ASFC, akidai kuwa imekuwa ngekewa kwake kufanya vizuri kwenye michauano ya kimataifa na michuano ya ndani.

“Huu ni msimu bora sana kwangu, kwa sababu tangu nianze kucheza mpira, kwenye mashindano ya kimataifa sijawahi kufunga mabao 7 au 6, nilikuwa nikiishia mabao 2 au 3.

“Hii inaonyesha kwamba ni msimu bora sana kwangu. Ninamuomba Mungu niendelee kufanya vizuri mpaka mwisho wa msimu,” amesema Mayele.

Mayele kwa sasa anaongoza kwa mabao katika Ligi Kuu bara akiwa na mabao 16, anaongoza pia kwa mabao kombe la Shirikisho Afrika akiwa na mabao 6 huku pia akiwa amefunga katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: