Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele, Bangala, Djuma watemwa Young Africans

Yanga 2023 24 Kikos kamili cha Yanga 2023/24

Sat, 22 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni dhahiri kuwa wachezaji watatu waliofanya vyema na Yanga katika misimu miwili iliyopita beki Djuma Shaban, Kiungo Yannick Bangala na Mshambuliaji Fiston Mayele hawatakuwa Yanga katika msimu ujao 2023/24.

Hiyo inathibitika baada ya hii leo Julai 22, Yanga kutangaza kikosi chake kamili kitakachoanza msimu mpya wa Mashindano 2023/24 huku majina ya wachezaji hayo yakiacha kutajwa.

Yannick Bangala na Djuma Shaban wao tetesi zinasema wanataka kutolewa kwa mkopo kwa kuwa mikataba yao inamalizika mwaka 2024.

Huku kwa upande wa mshambuliaji Fiston Mayele taarifa zikisema ameuzwa kwenda katika klabu ya Pyramids FC ya nchini Misri baada ya kufanya vyema katika Michuano ya Afrika msimu uliopita ma kuvutia vilabu vingi Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: