Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maxi atakuwa staa wa Ligi, atamfunika Skudu

Maxi Nzengeli X Congo Maxi atakuwa staa wa Ligi, atamfunika Skudu

Fri, 28 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Saleh Ally 'Jembe' amesema kuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga SC raia wa Congo DR, Maxi Nzegeli atakuwa staa mkubwa kwenye Ligi ya Tanzania tofauti na wanavyomtaja Skudu Makudubela wa Afrika Kusini.

Jembe amesema hayo mara baada ya kuwaona wachezaji hao kwenye mchezo wa Tamasha la Siku ya Wananchi ililofanika Jumamosi iliyopita wakati yanga ikicheza na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

"Ninaamini kama Maxi hataumia, akawa fiti muda wote, basi atamfunika Skudu. Skudu namuona kama mchezaji ambaye leo safi, kesho nafuu keshokutwa hauyupo na baadaye anarudi tena, lakini Maxi ni mchezaji ambaye anacheza straight football, hana mbwembwe ana malengo anatakakutoa pasi au kupiga.

"Maxi ni mchezaji ambaye aweza kukusababishia faulo ndani au nje ya eneo la penati, huwezi kujua ni wakati gani atatoa pasiu ama atapiga na ana kazsi. Kwenye kupiga anapiga na miguu yote miwili.

"Skudu sio mbaya ni mzuri, lakini namba zake hazionyeshi. Faida yake ni kwamba ni mzoefu zaidi na ametoka kwenye ligi kubwa ambayo ina kasi sana kuliko ligi yetu Tanzania.

"Ninamuona anaweza kutamba sana lakini ninataka nikwambie Maxi anakwenda kuwa staa mkubwa kuanzia Yanga yenyewe mpaka ligi yetu kwa ujumla," amesema Saleh Jembe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: