Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matola amuonya Miquissone "Usiishi kwa mazoea"

Matola X Miquissone Matola: Miquissone anakazi ya ziada Simba

Fri, 28 Jul 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati kilele cha siku ya Simba kikikaribia na mashabiki wakiwa na hamu ya kumuona winga wao wa zamani Luis Miquissone akitua uwanjani, Kocha wa vijana wa timu hiyo Seleman Matola asema bado mchezaji huyo anakazi ya ziada.

Miquissone aliyeuzwa na klabu hiyo mwaka 2020 na kwenda Al Ahly na kuacha pengo kubwa katika kikosi hicho.

Winga huyo amerejea tena katika kikosi hicho akiwa amemalizana na mabosi zake hao na msimu ujao watakuwa akichezea wekundu wa msimbazi.

Seleman Matola aliyekuwa kocha msaidizi wa kikosi hicho alisema kurudi kwa mchezaji huyo kumerudisha furaha ya kila mwanachama wa Simba kwani alitolewa kishingo upande.

Aidha alisema Luis anakwenda kukutana na changamoto kuwa ya namba ukizingatia vitu vingi kama kocha na wachezaji ni wageni.

Aliendelea kusema kuwa mapokezi makubwa aliyopewa haimanishi kuwa ataishi kifalme kikosi ila anatakiwa kujua kuwa ana deni kubwa.

“Hakuna linalishindikana ila Luis anatakiwa asiishi kwa mazoea kwa Simba imebadilika na Kocha hataruhusu kumchezesha mtu wa kiwango cha kawaida.

“Simba imefanya usajili mkubwa ambao hauwezi kumpa amani mchezaji yoyote kujiona ananafasi ya kucheza wakati wote kwani kila mtu ni bora,” alisema Kocha mkuu wa vijana Selemani Matola.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: