Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matawi ya Yanga yana nguvu kuliko Simba - Mchambuzi

Mashabiki Wa Yangaa Matawi ya Yanga yana nguvu kuliko Simba - Mchambuzi

Fri, 15 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia runinga ya TV3, Boiboi Mkali, amesema kuwa matawi ya Klabu ya Yanga yana nguvu zaidi nchini kuliko klabu yoyote ile.

Boiboi amesema hayo kufuatia vilabu vya Simba na Yanga kuhamasisha na kubeba baadhi ya mashibi zao na kwenda nao kwenye nchi ambazo watacheza michezo yao ya ugenini ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba imeondoka na mabasi 3 kwenda nchini Zambia ambapo watamenyana na Power Dynamos ya wakati Yanga ikiondoka na mabasi makubwa na madogo takribani 20 kuelekea Rwanda ambako watamenyana na Al-Merrikh ya Sudan, mechi zaote zitapigwa kesho Jumamosi, Septemba 16, 2023.

"Kwa sasa hivi matawi ya Klabu ya Yanga ndio matawi yenye nguvu zaidi nchini kuliko matawi ya klabu nyingine yoyote na hii huwa inatokea kutokana na mafanikio ya timu,kuna kipindi Simba walikuwa na nguvu sana.

"Japo kuwa kwa Yanga wao ni tofauti hata wakipitia kipindi kigumu bado wanaisapoti timu yao hata kipindi kile cha bakuli bado waliendelea kuipa sapoti timu yao," amesema Boiboi Mkali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: