Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa Yanga kamili kuwavaa Marumo Gallants

Kikosi Le Yanga Mastaa Yanga kamili kuwavaa Marumo Gallants

Tue, 9 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ally Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya nusu fainali.

Ni dhidi ya Marumo Gallants kutoka Afrika Kusini ambao usiku wa kuamkia leo Mei 9,2022 wamewasili ndani ya ardhi ya Dar.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Mei 10, Uwanja wa Mkapa Yanga wakiwa wenyeji kabla ya kuelekea Afrika Kusini kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili itakayoamua mshindi wa jumla kuelekea hatua ya fainali.

Kamwe amesema wachezaji wapo tayari na wanatambua umuhimu wa mchezo huo ambao utakuwa ni mgumu.

“Wachezaji wapo tayari na kila mmoja anatambua umuhimu wa mchezo huo ambao utakuwa ni mgumu kwa timu zote na tutafanya kazi kutafuta matokeo.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu yao kwa kuwa ipo kwenye mashindano ya kimataifa ambayo ni makubwa ni muhimu kuendelea kuwa bega kwa bega uwanjani na dua pia,” amesema Ally Kamwe.

Wachezaji wa Yanga wapo kambini wakiendelea na mazoezi na miongoni mwa wachezaji hao ni pamoja a Fiston Mayele, Aziz KI, Mudhathir Yahya, Salim Aboubhakari, ‘Sure Boy’, Kenedy Musonda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: