Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa Simba waingia vitani

Mastaa Simba SC Mastaa Simba waingia vitani

Wed, 2 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Pale Simba kuna jamaa wana rekodi za aina yake na majina yao yamekuwa mazito, je, nani atatoboa kuibuka staa wa timu na kipenzi cha mashabiki kwa msimu ujao unaotarajia kuanza Agosti 15.

Mwishoni mwa Ligi Kuu Bara msimu ulioisha, jina la mshambuliaji Said Ntibanzokiza ‘Saido’ lilipata nguvu kubwa mbele ya mashabiki baada ya kuingia kwenye ushindani wa kuwania kiatu cha ufungaji bora na aliyekuwa straika wa Yanga, Fiston Mayele.

Saido alilingana mabao 17 na Mayele ingawa alikuwa na cha ziada ambacho ni asisti 12, ambapo alipata tuzo ya mfungaji bora, kiungo bora na kikosi bora.

Kabla ya Saido msimu ulioisha huko nyuma jina la Clatous Chama kabla ya kwenda Barkane ya Morocco alikuwa amefunga mabao manane na asisti 15 na aliwahi kuibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu na umuhimu wake kikosini ni mkubwa.

Kuongeza kwa Luis Miqussone msimu huu ambaye kabla ya kuuzwa kwenye klabu ya Al Ahly ya Misri, akiwa ameifungia Simba mabao tisa na asisti 10 kunaongeza ushindani zaidi wa nani atakuwa kipenzi cha mashabiki ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao.

Mastaa wengine ambao wanaingia kwenye kinyang’anyiro cha staa wa timu ni Jean Baleke (mabao manane) aliyoyafunga nusu msimu maana alisajiliwa dirisha dogo na Moses Phiri (mabao 10) na asingeumia huenda angefunga mengi zaidi kama anavyosema kipa mpya wa Singida Fountain Gate, Beno Kakolanya.

Kakolanya alichambua Phiri jinsi alivyokuwa anamuona aina ya upigaji wake , mikimbio yake mazoezini na alikiri isingekuwa kupata majeraha anaamini nagekuwa mfungaji bora.

“Kama kuna kitu kikubwa wamekifanya Simba ni kumbakiza Phiri, ni hatari kulisoma goli, nimecheza naye pamoja mazoezini anachokifanya ndicho anakifanya wakati wa mechi, wachezaji kama hao ni adimu sana,msimu ulioisha asingeumia angekuwa mfungaji bora,”alisema.

Beki wa zamani wa Simba na Yanga, Amir Maftah alisema; “Kila mchezaji ana rekodi zake, hivyo lazima watapambana kwa kila namna kuhakikisha kila mmoja analinda heshima yake, hilo litafanya timu iwe na ubora mkubwa sana, wote uliowataja wameonyesha uwezo mkubwa ingawa umemsahau mzawa John Bocco lazima apewe heshima yake,”alisema.

Simba imepania kurejea kwa nguvu kwenye mashindano yote kwa kuanzia na siku yao wikiendi hii Kwa Mkapa.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: