Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa: Simba nunueni watano wapya

Simba 55Business Mastaa: Simba nunueni watano wapya

Wed, 10 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji wa zamani wa Simba wameitaka klabu hiyo kusajili wachezaji watano muhimu ambao ni mshambuliaji, kiungo mkabaji, beki wa kati, winga na beki wa pembeni mmoja ili waweze kutoboa kwenye michuano mbalimbali inayowakabili mwakani.

Simba juzi iliondolewa na Azam FC kwenye hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), kwa kipigo cha mabao 2-1 mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Kiwango cha timu hiyo msimu huu kimeonekana hakiwaridhishi mashabiki wa klabu hiyo licha ya kwamba kuna mechi wanashinda kwa mabao mengi lakini amepoteza taji hilo na ligi kuu bado wananafasi finyu kutokana na mtani wao Yanga anaeongoza msimamo akiwa na mechi tatu mkononi anahitaji pointi tatu tu kutetea taji.

Beki wa zamani wa Simba na Taifa Stars, George Masatu alisema; "Viongozi wa Simba wanaishi kwa kukariri wachezaji lakini hawaangalii timu inataka nini na kwa wakati gani. Hebu angalia kama beki wa kati anayetumika mara nyingi ni Inonga (Henock) na Onyango (Joash).

"Lakini kuna Kennedy Juma ni beki mzuri kama angeaminiwa kikosini kwani anapopewa nafasi anaonyesha kitu, Onyango amechoka akili inataka lakini mwili unagoma, wanatakiwa wawe na watu wa kubadilishana nao ingawa kwasasa hakuna anayeaminika zaidi kwenye safu hiyo zaidi ya hao wawili," alisema.

"Hata Inonga itafikia wakati atachoka na atafanya makosa kama ya Onyango ambayo yanatokana na mwili wake kuchoka. Simba waamke waende kutafuta wachezaji wa maana wasifanye usajili kiujanjaujanja, timu iwe na wigo mpana wa wachezaji kwa kila nafasi.".

Alisema safu ya ushambuliaji kuna Jean Baleke ambaye usajili wake umekuwa na tija kikosini lakini pia anahitaji msaidizi huku akimtaja Moses Phiri ambaye anasema anashindwa kutumika kutokana na kutoka majeruhi.

Winga wa zamani wa Yanga, Simba na Stars, Mrisho Ngassa alielezea kikosi cha Simba; "Wachezaji wengi hapa Tanzania wanashindwa kujitunza ili kufikia malengo makubwa, akifanya vizuri kidogo na kusifiwa basi analewa sifa na kushindwa kuendeleza pale alipoanzia.

"Hawa wanaokaa jukwaani kwa maana ya kutopata nafasi basi wanapaswa kujiongeza kwa kufanya mazoezi kwa bidii ili wanapopewa nafasi waonyeshe ubora wao lakini naona wengine wanafurahia kucheza Simba ama Yanga kwa vile ni timu kubwa pasipokujari kushuka kwa viwango vyao.

Hata hawa wachezaji wa kigeni kwa mfano Augustine Okrah na wengine naona usajili wao haukuwa sahihi maana hawana tofauti na wazawa wengine, na wanafurahia kuwepo Simba kwa vile ni timu kubwa Afrika ila hawana msaada wowote." alisema huku akisisitiza Simba kuachana na mastaa hao na kutafuta wachezaji watakaokuwa na tija kikosini.

Beki na nahodha wa zamani wa klabu hiyo, Boniface Pawasa alisema Simba inahitaji haraka kusajili mshambuliaji na kiungo mchezeshaji ili kuweza kuwasaidia waliopo katika mashindano yanayowakabili kwa sasa.

“Waongeze mtu mmoja wa kuwasaidia Baleke na Phiri ambaye anaonekana hana nafasi chini ya kocha sababu ukiangalia huko mbele wana mashindano mengi sasa kwa jinsi wanavyocheza sasa na bila kujipanga wanaweza wasitoboe ata msimu ujao;

“Tumeona baadhi ya wachezaji wakikosekana timu inayumba unaona kabisa timu inasumbuka kupata matokeo hivyo wanatakiwa pia kuongeza kiungo mshambuliaji mahiri pale kati ili aweze kuichezesha timu chama anapokosekana sambamba na nafasi nyingine ambazo hawana wachezaji mbadala,” alisema Pawasa na kuongeza;

“Pia ikiwezekana hata beki hasa wa kushoto wanatakiwa kuongeza ili kumsaidia Mohammed Hussein ’Tshabalala’ kwani kama mchezaji huyo atapata majeraha makubwa timu lazima ipate mtikisiko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: