Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa 23 Yanga waiwinda Marumo Gallants

Yanga Tizi Sad Mastaa 23 Yanga waiwinda Marumo Gallants

Tue, 16 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Usiku wa jana, Yanga imefanya mazoezi katika uwanja wa hoteli ya Royal Bafokeng iliyopo katika mji wa Rustenburg huku wachezaji 23 wakiandaliwa kuivaa Marumo Gallants katika mechi ya mkondo wa pili wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga inahitaji ushindi au sare kwenye mchezo huo utakaopigwa katika dimba la Royal Bafokeng kuanzia saa 12:00 jioni kwa muda wa hapa Afrika Kusini na saa 1:00 usiku kwa Tanzania ili iweze kutinga fainali ya michuano hiyo kwani ilishinda 2-0 uwanja wa nyumbani Benjamin Mkapa.

Mwanaspoti limekita kambi Rustenburg ili kukuletea kila kinachojiri, na katika mazoezi ya leo usiku kimeshuhudia wachezaji 23 wakifanya mazoezi chini ya benchi la ufundi linaloongozwa na Nassredine Nabi.

Mazoezi hayo yamefanyika kwa muda wa saa moja, yakihusisha mbinu, kunyoosha viungo na kucheza mipira ya kutenga (faulo na kona).

Kabla ya mazoezi haya ya usiku, asubuhi mastaa hao 23 wa Yanga walifanya mazoezi ya viungo katika ‘Gym’ kubwa iliyopo ndani ya hoteli walipofikia.

Wachezaji hao ni Djigui Diarra, Eric Johora, Metacha Mnata, Djuma Shaban, Shomari Kibwana, Joyce Lomalisa, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, na Yanick Bangala.

Wengine ni Zawadi Mauya, Mamadou Doumbia, Mudathir Yahya, Salum Abubakari ‘Sure Boy’, Kharid Aucho, Kennedy Musonda, Fiston Mayele, Tuisila Kisinda, Clement Mzize, Jesus Moloko, Denis Nkane, Farid Mussa na Stephane Aziz Kii.

Yanga imefanya mazoezi muda huu ambao ni sawa na muda ambao mechi ya keshokutwa itapigwa ili wachezaji wazoee mazingira.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: