Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki msihofu Inonga yuko fiti na Jumapili yupo!

Inonga Musonda Mashabiki msihofu Inonga yuko fiti na Jumapili yupo!

Fri, 11 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imefahamika kuwa Beki wa kati wa Simba Sc Henock Inonga Baka, anatarajiwa kuwepo kwenye mchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii 2023 dhidi ya Young Africans keshokutwa Jumapili (Agosti 13, 2023) katika Dimba la CCM Mkwakwani, Tanga.

Inonga ambaye ni raia wa DR Congo aliumia bega wakati wa mchezo wa Nusu Fainali dhidi ya Singida Fountain Gate uliopigwa jana Alhamis (Agosti 10), wakati akigombea mpira na mshambuliaji Meddie Kagere.

Taarifa kutoka ndani ya Simba zimeipeneyezea TanzaniaWeb kuwa Inonga amerejea kwenye hali yake ya kawaida na sasa anaendelea vizuri baada ya kutolewa uwanjani jana kutokana na kadhia hiyo na nafasi yake kuchukuliwa na Kennedy Juma Wilson.

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema Inonga atafanyiwa uchunguzi wa kitabibu leo, Wanasimba watapewa taarifa kuhusu hali yake

"Ni kweli Inonga aliumia jana, alitoka uwanjani akiwa na maumivu makali sana ya bega. Alipatiwa huduma ya kwanza, sasa anaendelea vizuri. Kesho (leo) Madaktari watamfanyia vipimo kubaini ukubwa wa jeraha ili kuona kama atahitaji matibabu zaidi au la," alisema Ahmed.

Mashabiki wa Simba walikuwa na taharuki juu ya uwepo wa beki huyo kisiki kwenye mchezo huo muhimu dhidi ya watani zao Yanga baada ya kuonyesha kiwango kizuri kwa misimu miwili sasa huku kombinesheni yao ikinpoga baada ya ujio wa beki Mcameroon, Che Fondoh Malone.

Ikumbukwe kuwa, katika mchezo wa mwisho uliozikutanisha Simba na Yanga, Simba iliibuka na ushindi wa bao 2-0, mabao yakifungwa na Inonga pamoja na Kibu Denis.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: