Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki mnastahili pongezi, wachezaji pambaneni

Mashabiki Yanga Mil 130 Mashabiki mnastahili pongezi

Thu, 2 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muhimu sana kuwapa pongezi mashabiki kwa namna wanavyojitokeza kwenye mechi za kimatafa ambazo wawakilishi wa Tanzania wanatupa kete pale Uwanja wa Mkapa.

Huzuni na furaha huwa zinaishi kwenye mioyo yao hivyo wanastahili pongezi kutokana na kujitoa kwao kila wakati hakika ni moyo mzuri na unapaswa kuendelea.

Tuliona wakati Yanga wakishinda dhidi ya TP Mazembe wengi walijitokeza kuona namna gani wachezaji wataonyesha makali yao.

Ushindi wa Yanga ulikuwa ni chachu kubwa kwa mashabiki kuendelea kuwa bega kwa bega na timu kwenye mechi zake za kimataifa hili ni jambo linalohitaji pongezi.

Simba walivurunda Uwaja wa Mkapa lakini bado mashabiki waliongozana na timu mpaka Uganda kwenye mchezo dhidi ya Vipers.

Nini tena wachezaji mnataka kutoka kwa mashabiki? Jukumu linakuwa kwenu sasa kucheza kwa umakini na kuipa ushindi timu.

Wapo wachezaji ambao kila baada ya mechi uwezo wao unakuwa ni hafifu licha ya kwamba wanauwezo mkubwa hili ni baya.

Kuna wakati huwezi kuwa bora ipo wazi lakini ikiwa ni muda wako wa kuonyesha ubora fanya hivyo, benchi la ufundi ni muda wa kuendelea kuwakumbusha wachezaji kuwa bao linafungwa ndani ya sekunde moja hivyo kila muda ni lazima kuwa makini.

Mashabiki furaha yao ni kuona timu inashinda na kupata matokeo mazuri kila mmoja anatambua hilo na muda ni sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: