Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapro Simba wapewa tano

Onana Mess Chama.jpeg Mapro Simba wapewa tano

Thu, 10 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kiwango kilichoonyeshwa na mastaa wa Simba juzi katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Power Dynamos kimewakosha wadau hasa Willy Onana na Fabrice Ngoma huku wakimpa muda Luis Miquissone.

Jumapili iliyopita Simba ilikuwa na tamasha lao maarufu la Simba Day linalofanyika kila mwaka kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa huku mashabiki wao wakipata nafasi ya kuwaona mastaa wao wapya watakaoitumikia timu hiyo msimu huu 2023/24.

Mchezaji wa zamani ambaye kwa sasa ni kocha, Kenny Mwaisabula alisema wachezaji wote ni wazuri usajili ambao utawapa Simba manufaa makubwa katika mashindano yote wanayoshiriki.

Alisema aliona namna Fabrice Ngoma na Willy Onana walivyokuwa bora japokuwa ni mchezo mmoja kuwapima kwa kikamilifu, ila wameonyesha mwanga na kitu walichonacho.

“Simba imefanya usajili mzuri na kwa kiwango cha jana upande wa pili najua vichwa vinawauma ila ndio hivyo kuimba kupokezana, nawapa mechi nyingine kuwasoma zaidi ila kwa jana nimeridhika,” alisema Mwaisabula.

Aidha Mwaisabula alisema Luis yule aliyeondoka, sio huyu aliyerudi lakini hajamkatia tamaa na anampa muda anaamini atashangaza.

“Luis nadhani kukosa michezo mingi huko alikokuwa kumechangia uzito aliokuwa nao, hivyo ni wajibu wa kocha kumrejesha kama zamani na yeye kujituma zaidi,” alisema.

Tigana Lukinja mchezaji wa zamani alisema usajili uliofanywa na Simba umezingatia vipaji sana hivyo kuwajaji kwa mechi moja atawaonea lakini uelekeo upo.

“Vipaji viko vingi pale Simba, sasa ni kazi ya kocha kuhakikisha anaviunganisha kupata kitu bora zaidi,” alisema Lukinja.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: