Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapema tu! Gamondi aanza kuwasoma Simba

Gamondi Ms Gamondi aanza kuwasoma Simba

Thu, 10 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi raia Argentina ni kama amempotezea kocha wa wapinzani wake wa kubwa wa Ligi Kuu Bara Simba, Robert Oliveira ‘Robertinho’ kwa kusema hawezi kuwapa presha wachezaji wake kwa ajili ya timu hiyo kwa kuwa siyo wapinzani wao pekee katika ligi.

Gamondi ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja tangu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kupitia Bodi ya Ligi kuachia ratiba ya michezo ya Ligi Kuu Bara msimu huu ambapo timu hizo zimepangwa kucheza mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara Novemba 5, mwaka huu.

Akizungumza nasi, Gamondi alisema kuwa, hawezi kuwapa presha wachezaji wake kwa ajili ya kuwaangalia wapinzani wao hao, kwa kuwa wana timu nyingi ambazo wanapaswa kucheza nazo katika Ligi Kuu Bara na kuweza kupata matokeo yatakayopelekea wao kuweza kutwaa ubingwa.

“Suala la kuwaangalia hilo ni jambo la kawaida kwa sababu wao ni mmoja kati ya wapinzani wetu ambao lazima tutacheza nao, ila hatupaswi kuwahofia kuna timu nyingine ambazo tutacheza nazo, kwa nini hofu iwe kwa wao pekee.

“Simba kwetu ni kama wapinzani wengine, tutaenda kucheza nao kutokana na mpango ambao utakuwepo kwa wakati huo na siyo kuhofia, hatuwezi kujenga timu ya kutaka kushindana na timu mmoja kwenye ligi, malengo yetu ni kushindana na kila timu ili kuweza kuchukua ubingwa wa msimu huu,” alisema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: