Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manula aweka rekodi ya kibabe CAF

Simbasctanzania Manula Aishi Manula

Tue, 21 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula pamoja na safu yake ya ulinzi wameweka rekodi yao ndani ya mashindano ya kimataifa katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kucheza mechi tatu mfululizo bila kutunguliwa.

Mchezo wa kwanza Februari 11, ugenini ubao uliposoma Horoya 1-0 Simba, Manula alifanya kazi kubwa ya kuokoa penalti kwenye mchezo huo licha ya timu hiyo kuyeyusha pointi tatu.

Dhidi ya Raja Casablanca alikwama kuokoa na alitunguliwa mabao matatu likiwemo moja la penalti na kufanya katika mechi mbili awe ametunguliwa mabao manne pekee ndani ya dakika 450.

Februari 25, 2022 Vipers 0-1 Simba kisha ule mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa Machi 7, Simba 1-0 Vipers na kete ya tano ilikuwa ni Machi 18, 2023 ubao uliposoma Simba 7-0 Horoya.

Ndani ya mechi tatu mfululizo ambazo ni dakika 360, Manula hajatunguliwa kimataifa huku safu yake ya ulinzi chini ya Joash Onyango na Hennock Inonga ikiwa haijatengeneza penalti nyingine kama mechi mbili za mwanzo.

Simba inafikisha pointi tisa ikiwa imekata tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya kuanza kwa mwendo wa kinyonga kwenye kundi C.

Kituo kinachofuata ni dhidi ya Raja Casablanca mchezo unaotarajiwa kuchezwa Machi 31ambapo Simba itakuwa ugenini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: