Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara awapa Simba masharti mawili kumuaga Mkude

Manara Mkude Ccc Jonas Mkude na Haji Manara waliwahi kufanya kazi pamoja wakiwa Simba SC

Thu, 13 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Jana Julai 12 Klabu ya Yanga kutangaza kumsaini Kiungo Jonas Mkude aliekulia katika Klabu ya Simba SC.

Ile kauli ya Simba kutaka kumuaga mchezaji huyo kwa heshima ni kama inaonekana kuwa ngumu hivi sasa baada ya kuachana nae mwishoni mwa msimu uliopita.

Simba ilitangaza hadharani kupitia kwa Msemaji wake kuwa inajiandaa kumuaga Kiungo wao aliedumu Klabuni hapo kwa miaka 13 kwa heshima kubwa katika tamasha lao la Simba Day.

Sasa utambulisho wa Mkude Yanga huenda unakwenda kufuta zoezi hilo lakini aliekuwa msemaji wa Yanga, Haji Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram aewapa Simba masharti ya kumuaga Mkude.

Manara ameandika

"Nimeona Somewhere, Afisa habari wa Madunduka akisema wamepanga kumuaga kwa Parade mchezaji wetu.

Yanga hatuna shida ya yeye kuja kuagwa siku ya Makolo Day, Tutashkuru mkimpa hiyo heshma Mchezaji wetu.

Ila inabidi muombe kwa maandishi na yasipungue maneno Elfu moja kwenye barua yenu ya maombi, na lazma hilo andiko liandikwe na Anko Mudi mwenyewe!!

Sharti la Pili aje kuagwa akiwa amevaa Jezi ya Yanga tena ile ya Njano,mkiweza hayo masharti atakuja kuagwa, na ieleweke atakuja huku akisindikizwa na Wananchi Elfu moja uwanjani Siku hiyo, wote wawe wametinga Jezi zetu.

Otherwise mchukueni huyo Nungu Nungu hapo juu, mumuage On Behalf of Him.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: