Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara: Azam kwa nini mnambebesha Fei Toto Juice za Timu?

Fei Manara X Manara Manara: Azam kwa nini mnambebesha Fei Toto Juice za Timu?

Thu, 10 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa mMsemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara katika hali ya utani amewakumbusha Azam FC kuwa watakuja kujuta kwa kitendo chao cha kumbebesha Maji Kiungo Feisal Salum "Fei Toto".

Ishu nzima ipo hivi;

Azam FC walitua Tanga juzi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa mtoano wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga mchezo uliopangwa kupigwa Uwanja wa Mkwakwani.

Sasa wakati msafara wa Azam ukiwasili, wachezaji wa Azam walifika Hotelini na wakati wa kushuka baadhi ya wachezaji walionekana wamebeba katoni za maji kwa matumizi ya timu mmojawapo akiwa ni Fei Toto.

Sasa katika utani wake kwa Fei Toto akaandika andiko kwenda kwa Azam na Fei Toto, ambapo aliandika;

Azam Fc mnaitafuta nongwa ya kiunguja sasa, Why mumbebeshe Juice zetu tamu? Zanzibar finest Feisal Salum ?

Hakawii huyo baadae kusema alikuwa anakuna nazi za @officialbakhresagroup Food ? Au mmesahau Ugali na Sukari?

Ngojeeni aondoke kama hajawaambia mlikuwa mnambebesha mizigo yote ya Team na alikuwa anaendesha yy Boti za Azam Marine"

Una neno hgani kwa Manara juu ya utani wake kwa Fei Toto?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: