Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama: Fei Toto alikuwa anakula ugali na sukari Yanga

Fei Toto Mhg Mama: Fei Toto alikuwa anakula ugali na sukari Yanga

Thu, 2 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mama mzazi wa aliyekuwa mchezaji wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amnedai kuwa mwanaye huyo amenyanyasika akiwa ndani ya Klabu hiyo ndiyo maana akaamua kuomba haki yake.

Mama Feisal amesema hayo ikiwa ni siku moja kabla ya maamuzi ya kamati ya Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kutolewa leo Alhamisi, Machi 2, 2023.

“Fei amedharirika sana mpaka hapa ilipofikia sasa ndio maana nimeona sio wakati wa kuficha ni bora niweke hadharani. Naomba TFF huyu mtoto imtendee haki yake, Fei imefika wakati wakati akawa anakula ugali na sukari, leo ndiyo nasema sasa. Kwa kutetea haki yake lakini alikuwa anaficha.

“Feisal ni mchezaji wa taifa, leo amekaa kama mtu aliyeua wakati anadai haki yake. Ilifika wakati anakwenda kwenye mazoezi na bodaboda na pesa ya kumlipa hana lakini kwa vile anafahamiana naye anamkopa.

“Inafika wakati anakosa hata pesa ya matumizi ananipigia simu kuniomba na mimi ninamtegemea yeye mengine siwezi kuyasema. Alikuwa anajituma kwa sababu ya ndugu zake.

“Nataka TFF wasome shitaka la Fei walisome kwa Kiswahili ili kila mtu ajue aliyoyapitia. Fei sasa hivi hana furaha na Yanga bora aondoke tu, mtoto kateseka sana. Amepambana kwa njia za kawaida kuwaomba wamuongezee maslahi yake lakini wakaona hana thamani,” amesema Mama Fei.

Ikumbukwe kuwa, Fei aliandika barua kuomba kuondoka Yanga lakini klabu iligoma hivyo akaamua kuondoka klabuni hapo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: