Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makaga: Yanga ni mahali salama, tutatembea kwa raha

Furahisha Pic Mjumbe wa Kamati Kuu ya Utendaji ya Yanga, Yanga Makaga akizungumza

Sat, 15 Jul 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Yanga, Yanga Makaga amesema klabu hiyo ndiyo sehemu salama kwa wachezaji na mashabiki kwenda na uongozi wa timu hiyo chini ya Rais, Hersi Said utahakikisha mashabiki na wanachama wanatembea kifua mbele kwa raha.

Makaga ametoa tambo hizo leo Julai 15, 2023 wakati wa uzinduzi rasmi wa tamasha la 'Wiki ya Mwananchi' kitaifa katika Uwanja wa Furahisha, Mwanza.

Makaga ametoa wasiwasi mashabiki baada ya kuondoka kwa Kocha Nasredinne Nabi kwani klabu hiyo ni kubwa barani Afrika na itaendelea kushusha majembe ya uhakika huku akiwaomba mashabiki kuwaunga mkono viongozi wao kwa kujiandikisha kwa wingi ili kuifanya klabu hiyo ijitegemee na kujiendesha kisasa.

"Wakati tunaingia madarakani tuliwaahidi raha na Wana Yanga leo wanatembea kwa raha kabisa hawana shida, tunawaahidi kwa ile safu ya uongozi tukiongozwa na Rais Hersi tumejipanga wote ni vijana tumejipanga kuhakikisha hampati presha, vidonda vya tumbo, na nyie mtusapoti kwa kujiandikisha kwa wingi kuifanya klabu yetu kuwa kubwa barani Afrika,"

"Mliona alivyoondoka kocha Nabi maombi tuliyopokea utafikiri ni Barcelona makocha wengi duniani waliomba, na yule wa kule aliomba lakini tulimuondoa. Tunawaahidi kwamba hatutowaangusha, muendelee kutuombea na kuwaombea wachezaji wetu, msimu utakavyoanza tutaendelea kutetema, na uongozi wa Yanga tutaendelea kushusha majembe ili msiwe na wasiwasi," amesema Makaga na kuongeza

Mjumbe huyo amesema katika kuhakikisha wanakuwa na timu za vijana imara, wamepanga kuendesha mchakato wa majaribio mikoani kupata wachezaji watakaounda timu zao za vijana chini ya umri wa miaka 20 na 17 ambao watagharamikiwa na wajumbe wa kamati tendaji a klabu hiyo.

"Sisi viongozi wenu tumejipanga tumeamua mwaka huu vijana wetu wenye vipaji kutoka mikoa yote watakwenda Dar es Salaam kufanyiwa usahili, tumeamua wajumbe wa kamati tendaji tutagharamika sisi kuwalea vijana hao watakapokuwa Dar es Salaam, huko nyuma vijana wetu walikuwa wanatoka Dar es Salaam tu kwahiyo tunawaomba mtusaidie kupata vijana hawa," amesema

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: