Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa: Yanga tayari, bado wenye nchi

IMG 4969.jpeg Majaliwa: Yanga tayari, bado wenye nchi

Sun, 23 Jul 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameshiriki mbio za NBC Marathoni huku akisema kilele cha wiki ya Wananchi kimepita inayosubiriwa ni siku ya wenye Nchi.

Jumamosi ,Julai 22,2023 klabu ya Yanga ilihitimisha kilele cha wiki ya mwananchi kwa kucheza na Kaizer Chief ya Afrika Kusini katika uwanja wa Benjamini Mkapa ambapo iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lilofungwa na Kennedy Musonda.

Akizungumza leo Jumapili Julai 23 katika mbio za NBC Marathoni katika uwanja wa Jamhuri Jijini hapa Majaliwa amesema baada ya mchezo wa jana sasa kinachosubiriwa ni siku ya Simba Day Agosti 6 mwaka huu.

“Niwakumbushe jana ilikuwa siku ya wananchi, Yanga inajiandaa kuingia katika ligi kuu,sasa tarehe 6 ni siku ya wenye nchi,nao wanajindaa, kuna wenye nchi na wananchi lakini kuna Azam, Namungo na Singida Big Stars hii yote ni hamasa iliyotolewa na NBC,”amesema Majaliwa

Waziri Mkuu ameipongeza benki ya NBC kwa kuandaa mbio huku akizitaka taasisi zingine kuiga mfano huo. Amesema Serikali inahitaji kuona kila taasisi ikipambana kuhakikisha sekta ya afya inazidi kuboreka nchini.

“Nitumie nafasi hii kuipongeza NBC kwa kuendeleza michezo piga makofi kwa NBC, watanzania mnajua benki hii ndio wadhamini wakuu wa ligi kuu ambayo ni ligi maarufu na inachukua nafasi ya tano, hizi ni jitihada za NBC,”amesema Waziri Mkuu

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi amesema kupitia mbio hizo jumla ya Sh300 milioni zimepatikana na zitaenda moja kwa moja kwenye matibabu ya kansa ya shingo ya kizazi kwa wanawake na kwenye taaluma ya ukunga nchini.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Pindi Chana amesema wamedhamiria kuwaondoa wagonjwa kwenye vitanda kwa kutumia mfumo wa ufanyaji mazoezi kuanzia ngazi ya mtaa.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: