Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa: Tuiombee Yanga irejee na Kombe

Kassim Majaliwa Bungeni Majaliwa: Tuiombee Yanga irejee na Kombe

Thu, 1 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka watanzania kuungana kwa pamoja kuiombea timu ya Yanga kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger utakaopigwa Juni 3, 2023 Algeria.

Akiwa bungeni Jijini Dodoma, Majaliwa amesema ni wakati wa Watanzania kuungana ili kuandika historia kwa pamoja na hana shaka na uwezo wa Yanga.

“Timu yetu ina uwezo mkubwa hivyo tuiombee, niungane na watanzania wenzangu kumshukuru Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kutoa usafiri kwa Yanga, Mwenyezi Mungu awatangulie ili wakaandike historia” Amesema Waziri mkuu

Yanga wameondoka hapa nchini leo Juni 1 kwenda nchini Algeria kwa ajili ya mchezo huo ambapo wanahitaji ushindi wenye faida kwao ili kuwa mabingwa wa kombe la shirikisho Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: