Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magazeti ya Afrika Kusini yaipigia chapuo Yanga

Yanga Squad Final Magazeti ya Afrika Kusini yaipigia chapuo Yanga

Tue, 16 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya magazeti ya hapa Afrika Kusini kwenye kurasa za michezo yameandika kuhusu Yanga kushinda ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC siku chache kabla ya mechi ya marudiano dhidi ya Marumo Gallants hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Tofauti ya timu hizi mbili [Yanga na Marumo Gallants] ipo hivi, Marumo Gallants inapigana kujinusuru isishuke daraja kwenye Ligi yake wakati Yanga yenyewe tayari bingwa kwenye Ligi ya Tanzania!

Kwa hiyo baadhi ya magazeti yamejaribu kuangalia tofauti ya timu hizi kwa upande wa Ligi zinazoshiriki na umuhimu wa mchezo kati yao.

Yanga ina mechi mbili za Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons huku tayari ikiwa bingwa lakini Marumo yenyewe ina mchezo mmoja dhidi ya Swallows wa Ligi ya Afrika Kusini ambao utaamua hatma yao ya kubaki Ligi Kuu au kushuka daraja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: