Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabeki Simba SC wakabana koo

Zimbwe Mohamed Tshabalala Mtwara Mabeki Simba SC wakabana koo

Mon, 15 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabeki wa pembeni wa Simba SC Mohamed Hussein Zimbwe Jr ambaye ni nahodha msaidizi na Shomari Kapombe, ngoma ni nzito ndani ya kikosi cha klabu hiyo kwenye upande wa kumwaga majalo.

Wote wawili ni namba moja kwa mabeki wenye pasi nyingi za mabao ambapo kila mmoja anazo sita kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2022/23.

Alianza Kapombe kugotea namba sita ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Young Africans uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa walipopata ushindi wa mabao 2-0 na kusepa na alama tatu mazima.

Zimbwe Jr alifuata ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ubao wa Uwanja wa Azam Complex uliposoma Simba 3-0 Ruvu Shooting.

Zimbwe kwenye ligi kacheza mechi 25, kasepa na dakika 2,318, Kapombe kacheza mechi 22, kayeyusha dakika 1,956.

Wamehusika kwenye pasi 12 za mabao, huku Kapombe akiwa ametupia mabao mawili kati ya mabao 66 yaliyofungwa na timu hiyo iliyo nafasi ya pili na alama 67.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: