Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lwandamina aitabiria ushindi Simba Sc Zambia

LWANDAMINA1?fit=700%2C400&ssl=1 Kocha George Lwandamina

Fri, 15 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Simba SC ikiwa nchini Zambia kwa ajili ya mchezo wa hatua ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos, Kocha Mkuu wa Zesco United, George Lwandamina ameipa nafasi ya timu hiyo ya Msimbazi.

Akizungumza kutoka Zambia, Lwandamina aliyewahi kuzifundisha timu za Young Africans na Azam FC, amesema mchezo huo hautakuwa mwepesi japokuwa anaipa nafasi kubwa ya kushinda Simba SC.

“Simba SC ina wachezaji ambao ni wazoefu żaidi kwenye michuano hii tofauti na Dynamos ingawa jambo kubwa ambalo limekuwa linawabeba ni kucheza kitimu kuliko kumtegemea mchezaji mmoja.” amesema.

Lwandamina ameongeza mabeki wa Simba SC wanapaswa kuongeza umakini sana pindi watakapokutana na mshambuliaji kinara wa timu ya Dynamos, Andy Boyeli kutokana na kufanya vizuri msimu uliopita.

“Boyeli alisajiliwa akitokea Klabu ya Chambishi na alijiunga nao katikati tu ya msimu uliopita ila aliibuka kinara wa ufungaji bora na kama haitoshi alichukua tuzo ya mchezaji bora msimu.” Amesema Lwandamina

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: