Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Luis Miquissone atengenezewa ufalme mpya Simba

VIDEO: Tazama Luis Miquissone Alivyoanza Mazoezi Na Simba Luis Miquissone atengenezewa ufalme mpya Simba

Fri, 28 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi Simba, umeweka wazi kuwa, wale watu wanaobeza wao kumrejesha Luis Miquissone, watulie kwani watamshangilia huko mbeleni baada ya kushangazwa na uwezo atakaouonesha.

Winga huyo amerejea Simba baada ya kuvunja mkataba wake Al Ahly ambapo kabla ya kuondoa kikosini hapo, aliweka ufalme ndani ya Simba jambo ambalo kwa sasa watu wanatarajia kumuona akirejesha ufalme wake.

Akizungumza nasi, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmedy Ally, Alisema: “Wale ambao wanambeza Luis Miquissone kwa nini amechagua kurudi ndani ya Simba, ndio haohao ambao watakuja kumshangilia pale ambapo atakuja kufanya mabalaa yake.

“Kwetu sisi hatuna shaka na uwezo wa Luis Miquissone kwamba tuwe na hofu ya kumrudisha kwani tunatambua uwezo wake ni wa aina gani, Luis ni moja kati ya wachezaji wakubwa sana, na ndani ya Simba atawashangaza watu wengi.

“Kwa sasa niwaambie tu Wanasimba wote kuwa mnachotakiwa kufanya ni kuhakikisha wanakuja kwa wingi sana katika Tamasha la Simba Day kujionea ubora wa wachezaji wao na jinsi gani ambavyo tamasha linafanyika kwa ubora mkubwa sana,” alisema kiongozi huyo.

Kwa upande wa Luis ambaye msimu wa 2020/21 katika Ligi Kuu Bara alitoa asisti 9, amesema: “Nimekuja kwa ajili ya kufanya kazi na ninaamini kwa kushirikiana na wenzangu tutawapa furaha mashabiki wa Simba na kutimiza majukumu yetu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: