Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa mziki huu Yanga patachimbika

Metacha Diarra Mshery Kwa mziki huu Yanga patachimbika

Fri, 28 Jul 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Yanga iko kambini ikiendelea kujifua tayari kwa msimu mpya wa mashindano lakini kuna vita kubwa ya kuwania nafasi ya kikosi cha kwanza ambayo inaweza kumpa presha kocha wa timu hiyo Miguel Gamondi

Yanga tayari imeshatangaza kikosi chao cha msimu ujao, kitakachokuwa na wachezaji 25 huku staa wa 26 wakati wowote atatambulishwa akitarajiwa kuwa mshambuliaji raia wa Cameroon Emmanuel Mahop.

Makipa watatu

Yanga wasiwasi kwamba eneo la makipa mwamba atabaki kuwa kipa wao namba moja Djigui Diarra ambaye anashikilia tuzo ya kipa bora wa ligi kwa msimu wa pili pia mfululizo tangu atue nchini lakini kuna msala ataawachia wenzake wawili.

Msala ambao Diarra anauacha ni pale siku atakapokosekana ni nani atachukua nafasi yake kati ya Metacha Mnata na Aboutwalib Mshery ambaye ameshapona baada ya kukaa nje kwa muda kutoka na majeraha.

Metacha na Mshery wote ni makipa wa timu ya Taifa Stars huku wiwango vyao havijapishana sana mtihani ukibaki hapo kuwa nani atakuja kuwa kipa chaguo la pili.

Beki wa kulia wawili

Upande wa beki wa kulia nako kuna vita, tayari Yanga imeshjakubali kumpoteza beki Mkongomani Djuma Shaban ambaye kiwango chake hakijawavutia mabosi wa timu hiyo kuendelea naye kwa msimu wa tatu tena akisitishiwa mkataba.

Yanga tayari imeshamshusha beki raia wa Ivory Coast Kouassi Yao kuja kuchukua nafasi ya Djuma lakini pia kumpa upinzani mwenzake mzawa Kibwana Shomari ambaye Djuma alishindwa kumpoteza kwa kucheza kwa kiwango kikubwa.

Yao anatakiwa kupambana kuhakikisha anaonyesha tofauti kati yake na Kibwana ambaye mabosi wa Yanga na makocha wanataka kuona beki wa kigeni anafanikiwa kumshinda beki huyo mzawa.

Kushoto nako vita ya wawili

Kule beki wa kushoto nako kuna mkongwe Mkongomani Lomalisa Mutambala ambaye ameshaletewa mtu mpya beki wa kazi mzawa Nickson kibabage ambaye kazi anaijua vizuri huku umri ukimruhusu.

Yanga imempunguza beki mzawa David Bryson akionekana kushindwa kushindania nafasi na sasa amekuja Kibabage kuja kushindana na Lomalisa lakini pia wawili hawa wakiishi na kivuli cha Kibwana ambaye wakati wowote anaweza kuvushwa upande akaja kutimba na huku kwa kuwa ana mudu kama ilivyo pia Yao.

Pale beki ya kati moto

Kama kuna shughuli pevu kubwa basi ni kuchagua mabeki wawili wa kati watakaoanza ukizingatia eneo hili pia lina manahodha wawili mkuu na msaidizi wake.

Yanga ina mabeki wa kati nahodha mkuu Bakari Mwamnyeto, msaidizi wake Dickson Job, beki wa kazi mjeshi Ibrahim Hamad 'Bacca' na sasa wameletewa mtu wa kazi mwingine mpya Mganda Gift Fred.

Mabeki hawa wanne Yanga ina jeuri ya kutengeneza seti mbili za mabeki hao wa kati wanaoweza kucheza kwa kuendana ambapo Job akicheza na Mwamnyeto kisha Bacca kucheza pamoja na Gift lakini uamuzi wa nani ataanza hapo Gamondi atalazimika kukuna kichwa.

Kiungo wakabaji watatu

Pale chini kiungo ukabaji kuna watu watatu wa maana yupo kaka mkubwa Mganda Khalid Aucho huku pia wakiwemo wazawa Mudathir Yahya na Zawadi Mauya nani wa kuanza huo ni mtihani utakaoamuliwa na Gamondi na wasaidizi wake kutokana na ubora wa viungo wote akitakuwa kuanza mmoja.

Winga wa kulia kuna kazi

Shughuli nyingine itakuwa upande wa winga wa pembeni kulia hapa kuna vita ya Wakongomani wawili na mzawa mmoja ambapo kuna ingizo jipya Maxi Nzengeli ambaye atapigania nafasi na mwenzake Jesus Moloko huku Denis Nkane akifuatilia vita hiyo kwa akili.

Balaa la Maxi limeshaonekana katika dakika 45 za kwanza tu alizoichezea Yanga dhidi ya Kaizer Chiefs lakini pia Moloko hana vitu vingi akiwa anajua vita anayoipigana.

Kiungo mchezeshaji

Hapa nako kuna vita nyingine ambapo kuna watu watatu watakaowaingiza makocha vitani, wapo Salum Aboubakar 'Sure boy', likaletwa ingizo jipya Pacome Zouzoua akitokea pale ASEC Mimosas lakini pia unachotakiwa kufahamu Nzengeli pia hapa anapamudu vizuri tena anaupiga mwingi.

Utata wanaume hawa utabaki kwa Pacome na Nzengeli ambao wanaweza kuchezesha timu lakini pia kufunga nani ataamua wa kuanza hapa ni wao wenyewe watakavyojituma lakini pia akili ya makocha wao.

Namba tisa watatu

Yanga kama itamalizana na Mahop hiyo itakuwa ni vita kati yake na Mzambia Kennedy Musonda na kinda Clement Mzize ambaye atakuwa anawafuatilia kujua nani anakosea.

Kumbuka watatu hawa wanapigania nafasi iliyoachwa wazi na nguli Fiston Mayele kazi yao rahisi itakuwa ni moja tu kujua kutumia nafasi za kufunga atakayekosa ubora huo nafasi ameitupa na kumwachia mwenzake.

Namba kumi nako acha

Nyuma ya namba tisa kutakuwa na namba 10 lakini hapa kuna Stephanie Aziz KI, Crispin Ngushi lakini kuna watu wawili wanaweza kujikuta wanaangukia hapa na kuongeza vita mpya ambao ni Pacome na Nzengeli.

Pacome hili ndio eneo alilosumbua zaidi akiwa na ASEC msimu uliopita akiwa mpaka mchezaji bora wa Ivory Coast akijua kuchezesha timu na kufunga mabao anavyotaka kama ambavyo Nzengeli anavyomudu kwa baalaa alilolifanya pale Union Maniema alikotokea.

Aziz KI anatakiwa kujipanga upya kwani anaweza kupoteza tena nafasi ya kuanza kutokana na ubora wa Pacome na Nzengeli kama hataamka usingizini kwani wawili hawa wana balaa lao wakicheza hapo.

Winga ya kushoto kutakuwa hivi

Kule winga ya kushoto nako kutakuwa na watu wawili Mahaltse Makudubela 'Skudu' na Farid Mussa ambao wataingia vitani kuwania nafasi moja kucheza hapo.

Changamoto ya Farid ni moja tu kuwa na muendelezo wa kiwango chake lakini akiwa kwenye moto ni mtu mbaya lakini mkongwe Skudu naye haitakuwa rahisi kwake kupoteza nafasi akiwa tayari ameshajichukulia 'kijiji' chake cha mashabiki kutokana na ufundi wake wa miguu kwa kuchezea mpira

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: