Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa Feisal, maswali ni mengi kuliko majibu

Fei X640.png Kwa Feisal, maswali ni mengi kuliko majibu

Sat, 27 May 2023 Chanzo: Tanzaniawen

Kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' amewashtua wadau wa soka nchini baada ya kutumia akaunti zake za mitandao ya kijamii kutembeza bakuli la kusaka fedha za kumpeleka Mahakama ya Usuluhishi la Kimataifa la Michezo (CAS) ili kuiburuza Yanga iliyoshindwa kumuachia licha ya kuvunja mkataba.

Hapa chini ni maswali matano tata yaliyoibuka baada ya ujumbe huo wa kiungo huyo kutoka Zanzibar ambaye mkataba na Yanga unadaiwa kumalizika Mei mwakani akitaka achangiwe fedha.

MASWALI TATA

1. Kama Fei aliweza kuilipa Yanga Sh 112 Milioni wakati akitangaza kuvunja mkataba na klabu hiyo ni vipi sasa ashindwe kiasi cha Sh 60 Milioni za kupeleka CAS wakati fedha hizo alirudishiwa?

2. Inaelezwa Fei ameizuia akaunti yake kupokea mishahara na bonasi kutoka Yanga, kwanini azikatae fedha halali za jasho lake na kutegemea fedha za kuchangiwa na wadau wakati alijua ataenda CAS?

3. Kama ni kweli amegomea mishahara kutoka Yanga, je kwa siku hizo zote bila kupokea mishahara anaishi kwa fedha zinazotoka wapi, ilihali aliwahi kukaririwa kuwa alikuwa akiishia kwa shida?

4. Imekuwaje uamuzi wa kutaka kuchangiwa kwenda CAS uje saa chache baada ya Kamati ya Sheria na Nidhamu ya Yanga kutoa taarifa ya kumtaka aende mbele yao kujitetea kwa utoro kazini?

5. Kwanini kila Yanga inapokuwa na mechi ngumu na muhimu ndipo sakata ya kiungo huyo uibuka na sio kipindi kingine, je hili linatokea kwa bahati mbaya na nani waliopo nyuma ya sakata hilo?

Chanzo: Tanzaniawen
Related Articles: