Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuwapita hawa wanaume ujipange

Aucho Bangala Inonga Kuwapita hawa wanaume ujipange

Sat, 25 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kisasi ni haki, lakini msamaha ni bora zaidi kwenye ulimwengu huu ambao una ushindani mkubwa na kila mmoja anahitaji kuonesha uwezo wake.

Karibu kwenye ulimwengu wa soka ambapo Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira na Yanga inayonolewa na Nasreddine Nabi, wote wametusua mpaka robo fainali kunako michuano ya CAF.

Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na Yanga kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, hapa tunakuletea baadhi ya nyota ambao ukitaka kuwapita kimataifa lazima ujipange.

SADIO KANOUTE Kiungo raia wa Mali, yupo ndani ya Simba hana mambo mengi nje ya uwanja hata akiwa ndani ya uwanja macho kwenye mpira na lango la mpinzani.

Waliotaka kumpita walikutana na mikato ya kimyakimya kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika jambo lililofanya aonyeshwe kadi tatu za njano kwenye mechi tofauti, akakosekana mchezo dhidi ya Raja Casablanca.

Kibindoni ana mabao mawili, aliwatungua Horoya kwenye Uwanja wa Mkapa.

KHALID AUCHO Ngoma nzito akiwa uwanjani mbishi kinoma noma, US Monastir wanajua balaa lake kwa kuwa alikiwasha mwanzo mwisho jambo lililofanya aonyeshwe kadi ya njano. Huyu ni kiungo wa Yanga raia wa Uganda.

MZAMIRU YASSIN Kazi yake ni kuvuruga mipango ya wapinzani ndani ya uwanja, mabeki na washambuliaji anga la kimataifa wanajua moto wake. Katika mchezo dhidi ya Raja Casablanca licha ya Simba kutunguliwa bado alivuja jasho la haki. Horoyo wanatambua namna alivyowavuruga nje ndani huyu mwamba ambaye ni mzawa.

MUDATHIR YAHYA Ni fahari ya Yanga akiwa na bao moja kibindoni, akifungua busta kupitika kwake lazima wapinzani wajipange kwani ni mwendo wa kazikazi ndani ya uwanja.

Sio TP Mazembe pekee ambao wanajua balaa la kiungo huyu mzawa, alipewa muda wa kufanya kazi chafu mchezo dhidi ya Real Bamako aliwanyoosha mpaka akaonyeshwa kadi ya njano dakika ya 84 ugenini kwenye sare ya 1-1.

CLATOUS CHAMA Akiamua kucheza basi Simba lazima wapate ule udambwidambwi na kumpita huwa inakuwa sio rahisi kutokana na akili nyingi kichwani.

Akiwa ndani ya 18, Mzambia huyu hana papara zaidi ya kuzungumza kwa vitendo huku akilinda mpira wake mguuni.

Mabeki wa Horoya wana kumbukumbu bora kuhusu Chama namna alivyowavuruga na bao lake la tatu hakuwa na mambo mengi ndani ya 18 aliwavuruga kisha akawatungua wakati Simba wakishinda 7-0.

Ni mabao manne anayo kibindoni kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi na pasi yake ya bao ni moja.

SALUM ABOUBAKAR ‘SURE BOY’ Ni mtulivu akiwa uwanjani, hana papara kwenye kutoa pasi na kukaba japo sio sana lakini yupo imara.

Alivuruga ile safu ya ulinzi ya US Monastri na kuonesha uimara ndani ya uwanja kwenye msako wa ushindi walioupata Yanga wa mabao 2-0 Uwanja wa Mkapa, alipopewa dakika 88 kiungo huyu mzawa.

JOASH ONYANGO Chuma cha Simba kutoka Kenya, chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Roberto Oliveira, penalti zote mbili ambazo Simba iliruhusu chanzo ni Onyango.

Ile dhidi ya Horoya ugenini iliyookolewa na Aishi Manula pamoja na ile dhidi ya Raja Casablanca iliyozama nyavuni.

Kazi kubwa anafanya uwanjani kutimiza majukumu ya timu ambapo kumpita ukiwa na mpira lazima ujipange, ukiwa na spidi utampa kazi ngumu kukuzuia.

IBRAHIM HAMAD ‘BACCA’ Mzawa huyu yupo zake ndani ya Yanga, iwe mipira ya juu au chini, yeye yumo, mchezo wake wa kwanza kuanza kikosi cha kwanza ilikuwa dhidi ya US Monastri, alipiga kazi kwelikweli.

Kadi ya njano ilikuwa mali yake dakika ya 25 kutokana na mikato yake ya kimyakimya.

KIBU DENIS Nguvu nyingi akiwa kazini na spidi kama zote licha ya mashabiki kutomuelewa lakini kocha wa Simba anaelewa muziki wake. Mchezo dhidi ya Vipers ugenini alikiwasha na alionyeshwa kadi ya njano.

MOHAMED HUSSEIN Beki huyu mzawa amekuwa imara katika kupandisha mashambulizi na kuimarisha ulinzi ndani ya Simba, kumpita inawezekana kutokana na makosa ya kibinadamu lakini lazima ujipange.

DJUMA SHABAN Ni mzuri kwenye kupiga faulo na kona, hapitiki kirahisi kwenye eneo lake na amekuwa akitimiza majukumu yake kwa kushirikiana na wachezaji wenzake wa Yanga. Beki huyu ni raia wa DR Congo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: