Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuondoka kwa Mayele imekuwa faida kwa Yanga - Oscar

Mayele Bora Kuondoka kwa Mayele imekuwa faida kwa Yanga - Oscar

Thu, 31 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mzee wa Kaliua Baba Mzungu mchambuzi wa masuala ya Soka katika Kituo cha Wasafi Media, Oscar George Oscar amesema kuwa kuondoka kwa aliyekuwa mshambuliaji kinara wa Yanga, Fiston Kalala Mayele kumekuwa faida kwa kikosi hicho kwani sasa hawana wa kumtegemea hivyo wanafunga kila mchezaji na kuzalisha mabao mengi.

Oscar amesema hayo mara baada ya kushuhudia michezo mitatu mfululizo Yanga ikifunga mabao matano kila mchezo jambo ambalo halijawahi kutokea kwenye timu za Tanzania kwa miaka mingi.

“Kitu kinachowasaidia Yanga ambacho mwanzo hakikuonekana ni kwamba, misimu iliyopita Fiston Mayele alikuwa target man, hata mechi ambazo alikuwa chini au ukimkamata vizuri kuliko kuna namna unakuwa umeikamata Yanga.

“Kuondoka kwa Mayele ni kama kulikuwa kunapunguza haya mabao mengi sababu wachezaji walikuwa wakicheza huku wakimtazama ni wapi alipo Mayele, zinaweza kupelekwa nafasi mbili au tatu akafunga moja, akatetema na watu wakafurahi hiyo burudani.

“Huenda kuondoka kwa Fiston Mayele kumesababisha kuongezeka kwa haya mabao mengi yanayopatikana. Kwa sasa timu inacheza bila target man kule mbele, wakienda eneo la mwisho la kushambulia hakuna mtu mahsusi ambaye wanamlenga kupeleka mipira kwake.

“Ndiyo maana Aziz Ki anafunga, Maxi nzengeli, Musonda na wachezaji wengine, kwa hiyo kuondoka kwa Mayele kumekuwa na faida kwa Yanga na hasa kwenye idara yao ya ushambuliaji,” amesema Oscar Oscar.

Mayele ndiye alikuwa top scorer wa Yanga kwa misimu miwili mfululizo na mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC msimu uliopita akiwa na mabao 17 pia alikuwa mfungaji Bora wa Kombe la Shirikisho Afrika akiwa na mabao 7.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: