Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kumbe hamasa sio tatizo kabisa

Yanga Watinga Fainali.jpeg Kumbe hamasa sio tatizo kabisa

Sat, 27 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Tulikuwa tunadanganyana sana hapo nyuma kuwa kila kunapofanyika hamasa kuelekea mechi muhimu ya soka inayohusu timu ya Tanzania, basi timu hiyo inapoteza mechi hiyo.

Mifano iko mingi labda nikutajie kadhaa, wa kwanza ukiwa ni ule wa mwaka 2007 pale Taifa Stars ilipocheza na Msumbiji katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, kwenye mechi ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2008 ambapo licha ya hamasa kubwa kufanyika hadi Rais wa nchi wakati ule, Mheshimiwa Jakaya Kikwete kwenda uwanjani, tulipoteza kwa bao 1-0 na matumaini yetu ya kufuzu yakafa.

Mwingine ni mechi dhidi ya Uganda iliyochezwa Aprili mwaka huu ambapo licha ya kushinda ugenini dhidi yao na kufanya hamasa kubwa wakati wa maandalizi ya mechi ya marudiano, tulipoteza nyumbani na kuweka rehani matumaini yetu ya kufuzu fainali zijazo za Mataifa ya Afrika.

Basi ndio ikawa hoja ya baadhi ya watu kukwamisha mipango ya hamasa pindi timu zetu zinapokuwa na michezo ya kimataifa hasa ile ambayo ina uhitaji wa ushindi.

Wanapoona tu masuala ya hamasa yameanza, wanaibuka na kudai yatachangia kufelisha timu zetu na wakati mwingine wanapelekea hadi wengi kuamua kutoshiriki kwa hofu tu ya kutoonekana wamekuwa chanzo cha timu kufanya vibaya.

Cha ajabu, hawa wapinga hamasa huwa hawatukumbushi nyakati ambazo jambo hilo lilifanyika na timu zikafanya vizuri.

Mfano, kumekuwa na hamasa kubwa kwa mechi za Yanga za Kombe la Shirikisho msimu huu na hata Simba ilipokuwa inafanya vizuri kimataifa, hamasa pia ilikuwa kimya lakini wamejikausha kimya hawatukumbushi.

Tatizo bwana sio hamasa bali ni uwezo tu wa timu na wachezaji. Ukiwa na kikosi kizuri na imara utafanya vizuri iwe kuna hamasa au hakuna na ukiwa na timu isiyo nzuri,hauwezi kufanikiwa hata kama utafanya hamasa mwaka mzima.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: