Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kumbe! Morisson ndie aliefanikisha dili la Skudu kutua Yanga

Skudu Morisson Bernard Morisson na

Thu, 20 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa Zamani wa Klabu ya Yanga Bernard Morisson kwa namna moja ama nyingine ndie aliefanikisha dili la Mahlatse Makudubela "Skudu" kutua katika Klabu ya Yanga.

Dhana hiyo inakuja baada ya Morisson kutua nchini na kutembelea kambi ya Yanga iliyopo Mji wa Kigamboni na kukutana na mchezaji huyo na kukumbatiana kwa furaha.

Baadae Morisson alipost ujumbe katika kurasa zake za mitandao ya kijamii uliosomeka;

“Ni furaha ilioje... hakuna haja ya kuzungumza mengi kwa sasa. Baadae nitazungumzia jinsi ninavyojivunia kukuleta hapa. Nenda ioneshe Tanzania kile ulichonifundisha. Mimi ni shabiki wako namba 1. NAKUPENDA KIJANA WANGU.” ameandika Morrison kwenye ukurasa wake wa mitandao ya kijamii.

Morisson na Skudu waliwahi kucheza pamoja Ligi Kuu ya Afrika ya kusini katika Klabu ya Orlando Pirates msimu wa 2018/19.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: