Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kramo sasa amejipata Simba

Aubin Kramo Training Kramo sasa amejipata Simba

Fri, 1 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Winga mpya wa Simba kutoka Asec Mimosas ya Ivory Coast, Aubin Kramo hajaonekana uwanjani kwa muda mrefu na kuibua minong’ono. Lakini taarifa njema kwa mashabiki wa klabu hiyo ni kwamba jamaa alikuwa na majeruhi na sasa amepona na ameanza kupiga tizi na wenzake.

Kramo aliumia kwenye mazoezi ya kujiandaa na mechi za Ngao ya Jamii zilizopigwa jijini Tanga na Simba kubeba taji kwa kuifunga Yanga kwa penalti 3-1 baada ya dakika 90 kumalizika kwa suluhu na kumfanya akose mechi nne zikiwamo mbili za Ligi Kuu ambazo Simba ilishinda zote.

Simba ilianza kwa kuinyuka Mtibwa Sugar mkoani Morogoro kwa mabao 4-2 kisha ikaifumua Dodoma Jiji kwenye uwanja wa nyumbani jijini Dar es Salaam kwa mabao 2-0 na kukosekana kwa Kramo ambaye ni kati ya wachezaji wapya waliosajili kwenye dirisha linalofungwa leo, kuliibua maswali kwa mashabiki.

Awali, kupitia mitandao ya kijamii kuliibuka taarifa kwamba Kramo ni mzima, ila anabaniwa na kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’, lakini mabosi wa klabu hiyo wakakanusha na kudai ni maneno tu.

Daktari wa timu hiyo, Edwin Kagabo aliliambia Mwanaspoti jana kuwa Kramo aliumia mguu na sasa anaendelea vizuri.

“Alikuwa mgonjwa akapata muda wa kupumzika ili kurejea katika hali yake ya kawaida, ila sasa hivi ameanza mazoezi ya pamoja na wenzake,” alisema Dk Kagabo aliyefafanua ishu ya kucheza kwa kwa sasa kwa mchezaji huyo ipo mikononi mwa kocha aamue kumtumia katika mechi atakazomhitaji.

“Ishu ya kucheza kwa sasa ipo kwa kocha, lakini ni kwamba Kramo anaendelea poa na ameanza mazoezi, tatizo alililokuwa nalo limeisha,” alisema daktari huyo. Simba inajiandaa na mechi za raundi ya kwanza za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos ya Zambia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: