Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Konkoni anavyompa 'tuition' Musonda

Konkoni Musonda Konkoni anavyompa 'tuition' Musonda

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dakika 90’ za mchezo zimemalizika jana, Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga Africans wameibuka na ushindi wa bao 5-0 dhidi ya KMC.

Mchezo huo umepigwa katika dimba la Azam Complex Chamanzi Jijini Dar es salaam. Job, Aziz Ki, Konkoni, Mudathir na Pacome ndio waligawa dozi zote.

Waraka wa bingwa mtetezi Yanga Afrika umesomwa vizuri, umepokelewa, umeeleweka na tayari kwa ajili ya utekelezaji kwa Washindani wote, majina ya Waandishi ni Dickson Job, Stephen Aziz Ki na Pacome Zouzoua, Bingwa ametuma taarifa KMC anakuja nazo kwenye group lenu, easy.

Hii ndiyo maana ya straika, Hafiz Konkoni amempeleka kwa tuition kwa Kennedy Musonda. 'Umeletewa wapishi, unahangaika hangaika nini nje ya box? Kaa eneo lako funga goli'.

Straika kazi yako ni kufunga magoli, ishi maeneo ya kazi yako, Konkoni anaishi kwenye kazi yake, Musonda anaishi nje ya kazi yake muda mrefu (Nje ya box).

Konkoni ameingia akitokea Sub, dakika (4) baadae akafunga bao, kisha akatoa Assist kwa Mudathir. Ni ndani ya dakika (7) tu. ↗️ Konkoni in — 65 ⚽ Konkoni scored — 69' Konkoni Assisted — 76

Hata mechi dhidi ya ASAS Djibouti alifunga bao pia ila mwamuzi hakuona kama mpira ulivuka mstari wa goli.

Huyu mwamba akiwa fiti 100% anaweza kufunga magoli mengi hata kuliko Mayele, kwa nini? Yeye hachezi mbali na box, tofauti na Mayele na Musonda. Zile tap-ins na mipira ya kichwa atafunga sana.

Mechi ya kwanza Ligi Kuu ya NBC, bao la kwanza na pasi ya bao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: