Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Konkoni afungukia bao lake "Nitaliweka kwenye documentary"

Hafizi Konkoni Konkoni afungukia bao lake

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji wa Yanga, Hafiz Wontah Konkoni amesema kuwa haikuwa kazi rahisi kwake kufunga bao lake la kwanza akiwa na timu yake mpya ya Yanga kutokana na presha kubwa aliyokuwa nayo tangu amejiunga na mabingwa hao watetezi.

Konkoni ambaye ni raia wa Ghana amesema hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa kwanza wa Yanga wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC ambapo straika huyo alifanikiwa kufunga bao moja miongoni mwa mabao 5-0 ambayo Yanga ilishinda jana.

“Imekuwa ni historia kubwa kwangu, ninahitaji kwenda kuitazama vizuri na kui-document hii kitu, hisia ilikuwa kubwa sana, haikuwa rahisi kwa sababu presha kwangu ilikuwa kubwa sana. Kwa hiyo ilitakiwa kuibeba ile presha.

“Mashabiki wananitegemea sana na hasa wakiangalia kile alichokuwa akikifanya Mayele, wanategemea niwafanyie makubwa, kwakweli nakosa usingizi lakini wananipa shauku ya kufanya vizuri zaidi.

“Nimecheza soka kwenye nchi nyingi lakini hapa morali ya soka ni kubwa sana, watu wanakuja wanakusapoti hata kama mambo hayaendi vizuri bado watakusapoti.

“Wapo wengine wanakufata wanakwambia si mashabiki wa Yanga ni mashabiki wa Simba lakini wanakutia moyo. Ninaamini nitafanya vizuri zaidi kwenye mechi zijazo.

“Naamini Jumamosi watakuta mashabiki wengi hapa Chamazi kwenye mechi ya CAFCL dhidi ya ASAS FC kumtazama tena Hafidhi Konkoni, nawapenda sana Wananchi,” amesema Konkoni.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: