Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha wa viungo Yanga atua Orlando Pirates

Helmy Prof. Helmy Gueldich

Wed, 2 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyewahi kuwa kocha wa viungo wa Yanga, Prof. Helmy Gueldich amejiunga na timu ya Orlando Pirates inayoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini.

Helmey alikuwa sehemu ya benchi la ufundi la Yanga lililoshinda mataji sita katika misimu miwili mfululizo likiongozwa na Nasreddine Nabi.

Aliondoka Yanga baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu uliopita. Awali alikuwa kwenye mpango wa kutua Kaizer Chiefs na Nabi.

Hata hivyo mpango huo haukufanikiwa, Nabi amejiunga na FAR Rabat, mabingwa wa Ligi Kuu ya Morocco na Helmey sasa ametua Orlando ambao ni wapinzani wa Kaizer Chiefs.

Mafanikio ya Yanga katika michuano ya Kimataifa msimu uliopita yamewapa ulaji waliokuwa makocha katika benchi la ufundi.

Aliyekuwa Kocha Msaidizi Cedric Kaze yeye ni kocha mkuu wa Namungo Fc wakati aliyekuwa Kocha wa magolikipa Milton Nienov amerejea kwao Brazil sasa akiwa kocha mkuu wa moja ya klabu inayoshiriki Serie B nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: