Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha wa Simba kukutana na Yanga nusu fainali CAF

Kerr Myr Kocha wa Simba kukutana na Yanga nusu fainali CAF

Mon, 1 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unaemuona hapoanaitwa Dylan Kerr! Ndiye Kocha Mkuu wa Marumo Gallants ya Afrika Kusini, timu itakayocheza na Yanga kwenye hatua ya Nusu Fainali ya CAFCC.

Dylan Kerry amewahi kuifundisha Simba msimu wa 2015/2016 kisha akaenda Gor Mahia alikokaa mwaka mmoja halafu tangu hapo kaenda Afrika Kusini ambako yupo mpaka sasa na amepita timu 4 hii ya 5 (Black Leopards, Baroka, Tshakhuma, Moloka Swallows na sasa Gallants).

Mwaka 2021 wakati Kaizer Chiefs wanakuja kucheza na Simba mchezo wa marudiano wa CAFCL Dylan Kerry kipindi hicho akiwa Kocha wa Tshakhuma Tsha Madzivhandila alinukuliwa akiwatahadharisha Kaizer Chiefs kwamba ameishi Tanzania, anazijua Timu za Tanzania hivyo Kaizer Chiefs wasiingie Dressing Room kwakuwa Timu za Tanzania hasa Simba wako tayari kufanya chochote ili wapate ushindi.

Muhimu, Yanga wa-focus kwenye maandalizi y michezo yote miwili, wanao uwezo wa kufanya hivyo bila hata kushauriwa na ninawatakia heri Wananchi waweze kufika fainali na hata kutwaa Ubingwa wa CAFCC.

Cha ajabu sasa, Marumo Gallants wako nafasi ya 14 kwenye Ligi Kuu ya nchini Afrika Kusini lakini Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Tanzania Bara mpaka sasa wanaongoza ligi hiyo wakiwa na alama 68 na kuna uwezekano mkubwa wa kubeba taji hilo tena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: