Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha wa Azam afunguka kilichowaponza kwa Yanga

Dabo Youssef .jpeg Kocha wa Azam afunguka kilichowaponza kwa Yanga

Thu, 10 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu Azam FC, Youssouph Dabo amekubali matokeo baada ya timu yake kupoteza mchezo dhidi ya Yanga SC kombe la Ngao ya Jamii, Jijini Tanga kwa kufungwa bao 2-0.

Yanga imetumia dakika 5 tu kuamua mchezo huo kwa mabao ya kiungo mshambuliaji, Mburkinabe Stephane Aziz Ki dakika ya 85 na Clement John Mzize dakika ya 89.

“Tofauti ya wachezaji wa hizi timu mbili ni maturity (ukomavu), baadhi ya wachezaji wangu kwenye kipindi cha pili walikuwa na uoga na wengine hawakutimiza majukumu yao ipasavyo, hawakuwa vizuri mentality ni jukumu langu kuwaweka sawa kwa kila nyanja.

“Mechi imetupa nafasi na benchi langu kutupa somo zuri kuhusu kazi yetu, nitakwenda kujiuliza baadhi ya maswali kwa baadhi ya wachezaji.

“Nimeshawahi kupoteza mchezo wa kwanza na nikawa vizuri kwenye ligi, latokeo ya leo hayawezi kupoteza focus yetu kuelekea michezo ya ligi, ni nafasi nzuri ya kuboresha kikosi change ninaamini huko mbele Azam FC itakuwa bora," amesema Dabo.

Yanga sasa inasubiri mshindi wa mchezo wa leo kati ya Singoida Fountain Gate na Simba, ambaye atashinda watakutana kwenye fainali huku Azam akisubiri atakayeshindwa mchezo wa leo atakutana naye kwenye mchezo wa mshindi wa tatu.

MECHI 6 ZA MWISHO Yanga v. Azam

• Yanga SC 2:0 Azam FC

• Yanga SC 1:0 Azam FC

• Azam FC 2:3 Yanga SC

• Yanga SC 2:2 Azam FC

• Azam FC 1:2 Yanga SC

• Yanga SC 2:0 Azam FC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: