Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha USMA: Yanga walipata huruma ya mwamuzi

Abdul Benchikha Kocha Mkuu wa USM Alger, Abdul Benchikha

Tue, 30 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa USM Alger, Abdul Benchikha, amesema wazi kuwa licha ya timu yake kupata ushindi wa mabao 1-2 ugenini mbele ya Young Africans, ila kuna vitu hakuridhishwa navyo.

Benchikha amesema mwamuzi alikuwa bora mwanzoni mwa mchezo huo, lakini kipindi cha pili akabadilika na kuamua kuwa upande wa Young Africans kwenye baadhi ya matukio.

Kauli ya kocha huyo inakuja baada ya kukiongoza kikosi chake kupata ushindi huo katika fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa juzi Jumapili (Mei 28) Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es salaam.

“Kipindi cha pili mechi haikuwa nzuri upande wetu kwa sababu hata refa naye alianza kuonekana kupendelea timu ya nyumbani (Young Africans), hii ni kawaida ukicheza ugenini.

“Lakini nimecheza dhidi ya timu nzuri yenye wachezaji wenye vipaji kuanzia nafasi ya ulinzi, kiungo na ushambuliaji.

“Tunarudi Algeria lakini bado mechi haijaisha, ni asilimia 50 kwa 50. Bado tuna kazi ya kufanya Algeria kwa sababu katika mechi ya marudiano Young Africans hawana cha kupoteza, watacheza wanavyojua ili wapate matokeo mazuri,” amesema kocha huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: