Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Nabieh: Tukipata bao moja tu, Yanga wamekwisha

Osama Nabieh Kocha Osama Nabieh.

Sun, 24 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Al Merrikh ya Sudan, Osama Nabieh amesema kuwa watakwenda Tanzania na mpango mkakati wa kuishambulia Yanga ili waweze kupata matokeo chanya baada ya kupoteza mchezo wa awali.

Nabieh amesema hayo kielekea mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga kufuatia mchezo wa awali Yanga kushinda ugenini kwa bao 2-0 nchini Rwanda, weekend iliyopita.

Mchezo qa marudiano unatarajiwa kupigwa wiki Ijayo, Septemba 30, 2023 katika Dimba la Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

"Tumepoteza mechi yetu ya nyumbani,sasa tunakwenda kucheza ugenini tukiwa bado tuna matumaini makubwa.

"Hatuendi kupaki basi,kama wao Yanga walipata matokeo ugenini na sisi tunaweza kupata matokeo mazuri ugenini.

"Hatutaenda kukaa nyuma,tunakwenda kuwashambulia na kama tutapata bao Moja la Mapema naamini tutafanikiwa kutafuta matokeo mazuri," Alisema kocha wa Al Merrikh, Osama Nabieh.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: