Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Nabi arejea Yanga, awapa kazi mastaa wake

Nasreddine Nabi Tunis Kocha Nabi arejea Yanga

Mon, 10 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mtunisia Nasredine Nabi amerejea nchini baada ya mapumziko ya wiki mbili na jana ameanza kuinoa timu kuelekea mechi na Kagera Sugar keshokutwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Nabi hakuwepo Yanga ikipata ushindi mwembamba wa 1-0 mara mbili katika mechi mbili zilizopita ugenini na nyumbani katika michuano tofauti.

Kwanza ni ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, TP Mazembe kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika Jijini Lubumbashi Aprili 2 na baadaye Jumamosi dhidi ya Geita Gold katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu Azam Sports Federation Cup (ASFC). 

Baada ya mchezo wa Jumanne na Kagera Sugar Yanga itarejea kambini kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya watani, Simba SC Aprili 16.

Mara baada ya kuwasili kambini Avic Town, Kocha Nabi alikutana na wachezaji wake wote na kuwakumbusha wachezaji kuwa bado wana safari ndefu na ngumu ya kumaliza msimu huu haswa kutokana na mechi zilizobaki kwa sasa.

"Tuna mechi za ligi mbeleni ambazo zinakwenda kuamua malengo yetu ya msimu huu, ni majukumu yetu sisi Kama benchi la ufundi pamoja na wachezaji kujitoa kwa nguvu kuipigania Yanga. Nawataka wachezaji wangu wote Sasa wajitoe kwa nguvu kuanzia mazoezini hadi kwenye mechi hatuna muda wa kupoteza sasa hivi," amesema Nabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: