Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Nabi akiri pengo la Aucho na Fei Toto

FEISAL AND AUCHO Aucho na Fei Toto

Thu, 1 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amekiri kuwa kukosekana kwa baadhi ya nyota wake muhimu, Khalid Aucho na Feisal Salum ‘Fei Toto’ umekiathiri kwa namna flani kikosi chake kwani ni miongoni mwa wachezaji muhimu wa kikosi hicho.

Nabi ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wanahabari katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar kabla ya kuanza kwa safari ya kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya mchezo wa kwanza kumalizika kwa Yanga kufungwa bao 2-1.

Nabi ameongeza kuwa anao uhakika kutokana ubora wa kikosi chake, hivyo watapata matokeo chanya na kurejea na ubingwa huo nyumbani.

“Nikiri kwamba, kukosekana kwa wachezaji wawili muhimu, Khalid Aucho na Feisal Salum kumekiathiri kikosi chetu kwa namna moja ama nyingine kwani kila mchezaji ndani ya Yanga ana mchango mkubwa na ni muhimu kulingana na mchezo husika.

“Timu inapocheza na Aucho ni tofauti na asipokuwepo, sisemi kwamba viungo wengine hawana uwezo, hapana, Aucho licha ya kucheza kimbinu na tactically, lakini pia ana uzoefu mkubwa wa mechi kubwa, kwa hiyo tunaamini angetusaidia.

“Kwa sasa nitatumia viungo waliopo kwani wana uwezo mkubwa na wanafanya vizuri, tunaamini wakishirikiana vizuri wachezaji wote na kujituma kwa uwezo wao, tutapata matokeo mazuri ugenini. Yanga imefanya hivyo sio mara moja, ninawaamini wachezaji wangu, tutafanya vizuri,” amesema Nabi.

Aucho ameshindwa kucheza michezo miwili ya fainali ya Kombe la Shirikisho kutokana na sababu za kikanuni baada ya kupata kadi sita za njano katika michuano hiyo huku Fei Toto akiwa nje ya klabu kufutaia mgogoro na uongozi wa klabu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: