Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Monastir: Yanga watatoboa nusu fainali CAF

Darko Novic Mm Kocha wa US Monastir, Darko Novic

Fri, 24 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa US Monastir, Mserbia Darko Novic ameipa Yanga nafasi kubwa ya kutinga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho na akawapa nondo kadhaa.

Novic ambaye kwao aliipiga Yanga mabao 2-0, amesema ina mambo mazuri ambayo yanawabeba na wanapaswa kuyaongezea nguvu na kuyachukulia kama silaha muhimu na wasibezwe.

Akizungumza nasi, kocha wa klabu ya US Monastir amesema Yanga ina mambo (2) mazuri yanayowabeba na wananafasi kubwa ya kufuzu nusu fainali iwapo watayaongezea nguvu.

"Ubora wa kwanza wa Yanga wanaoongoza kundi letu ni uwepo wa kocha Nasreddine Nabi ambaye ameiweka Yanga mahali salama kimbinu na kwamba hata ukiwa mbele unaongoza kwa bao (1) unahitaji ubora kulilinda bao lako kwa kuwa Nabi ni kocha anayebadilika badilika"

"Tulipocheza na Yanga tukashinda (2-0) lakini muda wote hatukuwa na utulivu wa kuona kama tumemaliza mechi. Nawaheshimu sana (Yanga) kwa kuwa wanaonesha kuna kazi kubwa kocha wao amefanya.. Hata nilipokuwa nawafuatilia na kuangalia mechi zao sikuona kama kuna mchezo wamezidiwa umiliki wa mpira"

"Napenda wanavyocheza, wanakulazimisha, wakati wote wanataka mpira uwe katika miliki yao. Tulipocheza nao kisha kucheza na Tp Mazembe tuliona tofauti kubwa ilitosha kuona kwamba Yanga watakuwa washindani wetu wakubwa katika kundi letu"

"Silaha ya pili ya Yanga ni wale washambuliaji wawili kwenye eneo la mbele, yule namba 9 (Mayele) ni hatari anajua sana kufunga lakini pia anakasi. Kuna yule jezi namba 25 (Musonda) ndio tatizo zaidi, unapokuwa na washambuliaji wa namna ile wanawalazimisha mabeki kupoteza nidhamu yao kutokana na kasi yao. Kitu kibaya zaidi wanacheza kwa ushirikiano mkubwa"

"Kwangu mimi nawaona (Yanga) watafika mbali kama watabahatika katika droo kutokukutana na timu ngumu. Najiandaa kuwaona wanacheza NUSU FAINALI" amesema Darko Novic.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: