Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Kaze aaga rasmi Yanga

Kaze  212030 702x459.png Kocha Kaze aaga rasmi Yanga

Thu, 20 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa kocha msaidizi wa Klabu ya Yanga, Cedrick Kaze raia wa Burundi ameaga rasmi ndani ya klabu hiyo baada ya kumalizika kwa mkataba wake na kuondoka.

Kaze alisajiliwa Yanga Oktoba 2020 kama kocha mkuu wa Yanga kabla ya kuondoka Aprili 2021 na kisha kurejea tena Septemba 2021 na kuwa kocha msaidizi chini ya kocha muu Nasreddine Nabi.

Makocha hao wote wameachana na yanga baada msimu kumalizika na tayari Nabi ameshatangazwa kama kocha mkuu wa FAR Rabat ya Morocco.

"Imekuwa ni safari ya kuzimu, baada ya kukaa miaka 2 na nusu Young Africans na kushinda Mapinduzi Cup x2, Ngao ya Jamii x2, Mabingwa wa Ligi x2, Kombe la FA x2, Mshindi wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika.

"Sasa ni wakati wa kusema kwa heri na kuitakia Klabu ya Yanga kila la kheri, Wananchii Asante kwa msaada wako katika kipindi chote tukiwa pamoja.

"Kwa wenzangu katika benchi la ufundi, wafanyikazi kutoka Avic Town na kwa wachezaji, haingewezekana bila bidii yako na kujitolea kwako, kwa menejimenti chini ya Rais Eng Hersi Said, kazi yako bora zaidi imekuwa muhimu kwa mafanikio ya klabu, kila la kheri Wananchi," amesema Kaze.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: